Wafuasi wa Chadema wakiwa katika viwanja vya mahakama leo na watuhumiwa wa kesi ya kutaka kumumwagia tindikali mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazin Deo Sanga (CCM)
Chadema supporters were in court today on the grounds of suspected case of wanting pours acid MP northern province of Njombe Deo Sanga (CCM )
Chairman of the Party for Democracy and Development ( Chadema ) cut the Njombe Ally Mhagama alias Dr who crushes and two other promotion treat trial on charges of violence have threatened to close range CCM with acidic Njombe constituency MP and chairman of the CCM northern province Njombe Deo Sanga .
These cadres have brought Njombe district court today following the violence that occurred on February 3, this year in the neighborhood of SIDO Njombe emerge after violence between Chadema supporters who stormed into the CCM session .
Apart from the chairman 's other cadres who had tried and Award include Karonga ( 40 ) who could not make it there for what Told the Court be the next patient is Robert Shejamabu ( 24 ) a student of the University of Hope branch of Njombe
Prosecutor government Rizick Matitu reciting these charges before the judge in charge of the court Augostino Rwizile that on February 3, this year accused them together they make a mess in the neighborhood of Sidon for the sake of a breach of the peace contrary to section sherea 89 ( 1 ) ( a) of the penal code .
The prosecutor said the second charge is injected the solution menacingly Deo Sanga who is Executive Chairman of Njombe region law contrary to section 89 ( 1 ) ( b ) Chapter 16 of the penal code .
However, the two defendants in this case who came to Court when Ally Mhagama and Robert Shejamabu were denied the charges and released on bail , which the judge Rwizile adjourned the case until March 6, this year.
Due to the violence also two of the CCM supporters , Steward yoke ( 30 ), a resident of Njombe Urban and Henry Done ( 36 ), a resident of the district of Joshoni have appeared in court and read a single charge of assaulting a police officer with a phone hurt G. 305 David crush who arrived at the scene with the goal settling the argument.
Gracious public prosecutor before the judge Mpagama Rwizile that the defendants acted incident on February 3, this year in the neighborhood of Sidon against the passage of law 89 ( 2 ) (a ) of the penal code .
They were also accused denied the charges and are out on bail until March 6, this year the case is stated .
Limited choice of ward councilor in Njombe you expect to be held on Sunday this week to replace former ward councilor Lupiana Fute who died last year and the CCM and Chadema so strong I come into contact in the campaign
For Swahili Continue here
MWENYEKITI wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kata ya Njombe Ally Mhagama maarufu kwa jina la Dr Sagasaga na wenzake wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwafanyia vurugu wana CCM pamoja na kutishia kumumwangia tindikali mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga .
Makada hao wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Njombe leo kufuatia vurugu zilizotokea Februari 3, mwaka huu katika mtaa wa SIDO Njombe baada ya kuibuka vurugu kati ya wafuasi wa Chadema waliovamia kikao cha ndani cha CCM .
Mbali ya mwenyekiti huyo makada wengine waliofikishwa mahakamani hapo ni pamoja na na Award Karonga (40) ambaye hakufika mahakani hapo kwa kile kilichadaiwa kuwa ni mgonjwa mwingine ni Robert Shejamabu (24) mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini tawi la Njombe
Mwendesha Mashtaka wa serikali Rizick Matitu akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Augostino Rwizile kuwa mnamo Februari 3, mwaka huu washtakiwa hao kwa pamoja walifanya fujo katika mtaa wa Sido ambazo zingepelekea uvunjifu wa amani kinyume na kifungu cha sherea cha 89 (1) (a) ya kanuni ya adhabu.
Mwendesha mashtaka huyo alisema shtaka la pili ni la kumtishia kumwagia tindikali Deo Sanga ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe kinyume na kifungu cha sheria cha 89 (1) (b) sura ya 16 ya kanuni ya adhabu.
Hata hivyo washtakiwa wawili wa kesi hiyo waliofika mahakani hapo Ally Mhagama na Robert Shejamabu walikana mashtaka hayo, na kuachiwa huru kwa dhamana, ambapo hakimu Rwizile aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 6, mwaka huu.
Kutokana na vurugu hizo pia wafuasi wawili wa CCM, Steward Mkongwa (30) mkazi wa Njombe Mijini na Henry Ndone (36) mkazi wa mtaa wa Joshoni wamefikishwa katika mahakama hiyo na kusomewa shtaka moja la kumshambulia na kumjeruhi askari polisi mwenye namba G. 305 David Mponda aliyefika katika eneo la tukio kwa lengo kusuruhisha ugomvi huo.
mwendesha mashtaka wa serikali Rehema Mpagama mbele ya Hakimu Rwizile kuwa washtakiwa hao walitenda tukio hilo Februari 3, mwaka huu katika mtaa wa Sido kinyume na kifungu cha sheria cha 89 (2)(a ) cha kanuni ya adhabu.
Pia washtakiwa hao walikana mashtaka yao na wako nje kwa dhamana hadi Machi 6, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.
Uchaguzi wa mdogo wa diwani wa kata ya Njombe mjini unataraji kufanyika siku ya jumapili wiki hii kuziba nafasi ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo Lupiana Fute aliyefariki dunia mwaka jana na vyama vya CCM na Chadema ndivyo ninavyopambana vikali katika kampeni hizo
No comments:
Post a Comment