Today , DATE February 24, 2014 I declare to change the leadership of the Wildlife Division of the Ministry of Natural Resources and Tourism as follows :
Professor Alexander Songorwa detaches work in the position of Director of the Wildlife Division of the Ministry of Natural Resources and Tourism.
I take this action because of my dissatisfaction with the performance of the department's work in the fight against poaching developing country.
In addition , this step is the implementation of the Resolution of the Parliament issued on 22 December , 2013 , set to the Director of Wildlife held responsible for allegations of negligence and violation of human rights in the eradication operation .
Implementation of this command starts immediately, and I namteua Lord Paul Sarakilya act that position of Director of the Wildlife Division of Natural Resources and Tourism visits from now.
In addition , I muondoka Professor Jafari Kidegesho in place of Assistant Director Sustainable Use of Wildlife and appoint Dr . Charles Mulokozi the role.
Even so , I appointed Lord Deputy Director Julius Bebe Prevention - Poaching and is replacing who may be acting Director of Wildlife.
Similarly , Mrs Ebbo China continues to be the Assistant Director of Training, Research and Statistics, and Mr. Herman Keiraryo keeps Development Assistant Director of Wildlife. Despite Prohibition Unit - Poaching I chokitaja earlier, these are the units of the Department of Wildlife in the Ministry of Natural Resources and Research.
Nawaagiza that all Directors and Heads of each department , every agency , and all institutions within the Ministry of Natural Resources and Tourism to make key indicators of performance (Key Performance Indicators ) nakukabidhi me within the next 30 days . These indicators are the steps to achieve the following objectives , 1 ) The objectives of the ministry , 2 ) Responsibility , 3 ) Uwazina 4 ) The effectiveness in the performance of daily tasks . It is a condition we can fulfill the ministry strategies in inayopimika systems , we can measure natuweze measured, National natutumikie with integrity .
To the staff of the Ministry of Natural Resources and Tourism , including myself, Lazaro Nyalandu , will have to consider and implement work assignments based on the Code of Conduct (Code of conduct ) that zitapendekezwa and approved by the Council of Employees of the Ministry. This Council should be limeitishwa and Secretary General of the Ministry before the end of next month . The purpose of these regulations is to be based on quality of service , responsibility , dignity , equality and justice in the execution of our daily tasks .
God bless Tanzania .
Thank you .
Lazaro S. Nyalandu ( MB )
Ministry of Natural Resources and Tourism
24/02/2014
**********************************************************************
WAZIRI WA MALIA SILI ATIMUA WAKURUGENZI WANYAMAPORI
Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo:
Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini. Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.
Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa.
Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo.
Hali kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Vilevile, Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utafiti.
Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) nakukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo. Viashiria hivi ni hatua ya kufanikisha yafuatavyo, 1) Malengo ya wizara, 2) Uwajibikaji, 3) Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku. Ni sharti tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu.
Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. Baraza hili liwe limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao. Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.
Mungu ibariki Tanzania.
Asante.
Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014
Asante.
Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014
No comments:
Post a Comment